Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Ndaki ametembelea kambi ya wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwamadulu.
Akiwa katika kambi hiyo Ndaki aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao wanayotarajia kufanya mwishoni mwa mwaka.
Alisema kuwa kufaulu kwa wanafunzi hao kutailetea sifa wilaya ambayo ufaulu kwa umekluwa ukiimarika mwaka hadi mwaka pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa.
Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu pia Mkurugenzi Mtendaji huyo alikagua miradi ya maendeleo shuleni hapo.
Miradi aliyokagua ni pamoja na matundu ya vyoo ambayo ujenzi wake unaendelea ambapo kukamilika kwake kutasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa changamoto ya uhaba wa miundombinu hiyo inayowakabili wanafunzi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa