Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Ndaki amewataka wataalamu kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ndaki alitoa maagizo hayo wakati akikagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika vijiji vya Mwamadulu, Lagana, Ngunga, Negezi, Igaga na Uchunga.
Ndaki alisema kuwa watalaamu hususan wa ujenzi wanapaswa kutembelea miradi hiyo na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kujiridhisha na namna inavyojengwa.
Aliwataka pia kuepuka kutokuelewana miongoni mwao kwa kuwa na lengo moja ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati badala ya kutofautiana jambo linalochelewesha maendeleo kwa wananchi.
Alisema Serikali inahakikisha miundombinu ya eliamu inaboreshwa na ndio maana inatoa fedha hivyo watendaji wahakikishe wanasimamia vyema ili miradi ikamilike kwa wakati.
Aidha pamoja na mambo mengine akiwa katika maeneo tofauti tofauti Mkurugenzi Mtendaji aliwaagiza wakandarasi kukamilisha miradi hiyo kwa walkati ili jamii ianze kupata huduma.
Katika ziara hiyo alikagua miradi ya ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo katika shule za Sekondari Mwamadulu na Lagana ambayo imeanzishwa ili kuongeza wigo wa utoaji huduma ya elimu.
Pia aliweza kufika katika shule za sekondari Igaga, Ukenyenge na Uchunga ambako miradi ya nyumba za walimu, vyoo pamoja na mradi wa zahanati ya Ngunga inayoendelea kutekelezwa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa