Na Ofisi ya Habari Kishapu
Hospitali ya wilaya ya Jakaya Kikwete imeanza rasmi kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa na wajawazito ambao hushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.Huduma hii imeanza kutolewa tarehe 23/02/2017,mpaka sasa jumla ya wagonjwa wanne wamekwisha fanyiwa upasuaji na hali zao za kiafya ziko vizuri na zinaendelea kuimarika vizuri.Kwa mujibu wa mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt Josephat Shani alieleza hospitali ya Jakaya Kikwete ilianza kutoa huduma kama hospitali ya wilaya mwezi Machi 2016 imekuwa ikitoa huduma kwa wagonjwa wa nje bila kutoa huduma za upasuaji kwa sababu ya ukosefu wa vifaa tiba na miundombinu isiyokuwa rafiki kwa huduma za upasuaji,kwa sasa miundombinu kwa kiasi fulani inakidhi kwa upasuaji mdogo na upasuaji kwa wajawazito alisema.
Aidha Dkt Shani aliendelea kufafanua kuwa hospitali hii inatoa huduma ya upasuaji kwa msaada wa wadau mbalimbali waliosaidia ujenzi wa miundombinu na vifaa tiba ,wadau waliosaidia vifaa tiba ni shirika lisilo la kiserikali la GOOD NEIGHBOURS na mgodi wa Williamson Diamond Limited.
Pamoja na mfanikio ya kuanza kwa huduma za matibabu ya kawaida katika hosipitali hii tunazo changamoto za upungufu wa madaktari 12, wauguzi 28 na wataalamu wa usingizi pia vifaa tiba kama mashine za mionzi ( X-ray na ultra sound),jenereta ya umeme wa akiba na chumba cha famasia.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa