Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeweka mikakati ya kupanda miti 9,000 kila mwaka ikiwa ni njia ya kuondokana na ukame unaoweza kusababisha jangwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Stephen Magoiga amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu maadhimisho ya upandaji miti kitaifa yaliyofanyika wilayani humo kwa muda wa siku tatu.
Mkurugenzi Magoiga alisema kuwa kwa kuanzia kila taasisi ya Serikali wilayani humo zikiwemo shule za msingi, sekondari na pia vijiji zitakuwa zinapanda miche ya miti na kuitunza.
“Inasikitisha sana kuona Kishapu inataka kugeuka kuwa jangwa na hili jangwa limetokana na mikono ya binadamu wamekata miti na kuimaliza sasa tutumie mikono hiyo kuirusha kwa kuipanda,” alisema.
Aliongeza kwa kudokeza kuwa mikakati iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya kishapu ni kuhakikisha kila mwananchi anapanda miti katika maeneo yake na kuitunza ili iweze kukua.
Alisema kuwa Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla itaweza kugeuka na kuwa ya kijani endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake katika kupanda miti.
“Ili kufanikisha haya yote tumeanzisha bustani katika shule ya Sekondari Shinyanga na Mwamashele na tunatarajia pia kuwa na bustani katika shule zote za Wilaya ya Kishapu na tutaenda hivyo hadi ngazi za vijiji,”
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa