MGODI WA ALMASI MWADUI,HALMASHAURI YA KISHAPU WATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO UTEKELEZAJI MIRADI YA CSR SH.BILIONI 1
MGODI wa Madini ya Almasi Mwadui Williamson Diamond (WDL)pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, wametia Saini hati ya makubaliano (MoU)ya utekelezaji wa Miradi 16 ya Maendeleo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) Sh.Bilioni 1. Utiaji Saini huo umefanyika leo Marchi 6,2024 Katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wanatoka kwenye vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi huo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,akizungumza wakati wa kufungua hafla ya Utiaji Saini, ameupongeza Mgodi wa Mwadui kwa kutoa fedha hizo za CSR, ambazo zitatumika kutekeleza Miradi Mbalimbali ya Maendeleo kwa wananchi. Amesema Mwaka Jana Mgodi huo ulitoa tena fedha za CSR Sh.bilioni 1.2 ambayo ilitekeleza Miradi Mbalimbali ya Maendeleo,na Mwaka huu wametoa tena Sh.bilioni 1 ambayo itatekeleza Miradi 16 ya Maendeleo.
"Fedha hizi zinakwenda kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambayo inaigusa Jamii, sababu imeibuliwa na wananchi wenyewe ikiwamo ya Sekta ya Afya,Elimu,Miundombinu ya Stendi na Barabara,"amesema Mkude. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya, amesema fedha hizo Sh.bilioni 1 kwamba asilimia 60 zitatekeleza Miradi ya kimkakati, na Asilimia 40 zitakeleza Miradi ya Maendeleo katika Vijiji 12 ambavyo vinazunguka Mgodi wa Mwadui.
Naye Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo, amesema wametekeleza Takwa la Kisheria kwa kutoa fedha hizo za CSR Sh.bilioni 1 ikiwa ni asilimia 0.7 ya pato ghafi. Aidha,ameiomba Serikali wakiwamo na Viongozi kutoka Vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi, kwamba waimalishe ulinzi na kuzuia uvamizi ndani ya Mgodi huo ili wasije kusitisha uzalishaji, bali waendelee na uzalishaji hali ambayo itaongeza mapato ya CSR.
Amewataka pia Wananchi ambao wanatekelezewa Miradi hiyo ya Maendeleo kwenye maeneo Yao kwamba waitunze ili itumike vizazi na vizazi. Mwenyekiti wa Vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi Mwadui Charles Manyenye, ameupongeza Mgodi huo kwa kuendelea kutoa fedha za CSR ambazo zimeendelea kuimarisha Mahusiano Mazuri Kati ya Wananchi na Mgodi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa