Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeanza kujenga na kuboresha miundombinu katika kituo chake cha afya kutokana na fedha sh. milioni 400 zilizotolewa na Serikali kupitia Benki ya Dunia (WB).
Kituo cha afya cha Songwa kilichopo kata ya Songwa kimekuwa mnufaikaji wa fedha hizo ambapo kinafanyiwa uboreshaji wa miundombinu yake ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji na maabara.
Miundombinu mingine ni ujenzi wa nyumba nyingine ya watumishi, chumba cha mama na mtoto pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisa Mipango Halmashauri ya wilaya hiyo, Mang’era Mang’era amebainisha hayo ambapo amesema kuwa zipo changamoto zinazoukabili mradi huo zikiwemo uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kuhusu kujitolea nguvu kazi.
Alisema wananchi hawaelewi dhana ya ushirikishaji wa jamii katika masuala ya miradi ya maendeleo huku wengine wakiamini ni Serikali pekee ndiyo itakafanya shughuli zote.
Mang’era alisema wanakabiliana nazo kwa kufanya vikao vya kuhamasisha jamii kutambua kuwa hii ni miradi ya yao na hivyo hawana budi kuchangia nguvu kazi kwani itakuwa na tija kwao.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa