Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye ubora na kwa gharama nafuu.
Pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa fedha kwa ajili ya uimarishaji wa vituo mbalimbali vya afya pamoja na sekta ya elimu.
Kabeho ametoa pongezi hizo jana kwa nyakati tofauti wakati akikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya mendeleo wilayani humo ambako Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa.
Sanjari na hilo Kiongozi huyo alipongeza wilaya hiyo kwa kuishirikisha jamii katika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya jambo ambalo linachangia uboreshaji wa sekta hizo.
“Kishapu mna kitu cha pekee tofauti na huko kwengine nilikopita, hapa ninyi katika miradi yenu mlipopewa fedha ndani ya gharama mmebakiza chenji na mnaongeza miradi mingine kwa fedha hizo hizo hivyo mnafanya kitu cha kuigwa,” alisema.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge aliongeza kuwa kwa kuishirikisha jamii katika utekelezaji wa miradi hali inayoifanya nayo ifanye uwekezaji wa maendeleo katika senkta mbalimbali.
Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” ulikabibidhiwa mkoani Shinyanga wilayani Kishapu ukitokea wilayani Maswa mkoani Shinyanga umepitia miradi ya sh.bilioni 2.2.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2018 zimebeba ujumbe “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” ukiwa umezingatia vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwashirikisha wananchi, wadau wa maendeleo na Asasi binafsi katika kuboresha miundombinu ya elimu na uhamasishaji wa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi mbalimbali watakaolisaidia Taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa