Hospitali ya Wilaya ya Kishapu ya Dk. Jakaya MrishoKikwete inatarajiwa kupata gari jipya la wagonjwa ‘ambulance’ ili kutatuachangamoto ya usafiri iliyokuwa ikiikabili.
Hayo yamebainishwa Februari 12, 2019 na Mkuu waMkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack wakati akizungumza kwenye ziara ya Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi wilayani humo.
Mhe. Telack alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwaalitoa msaada wa magari manne ya wagonjwa kwa Mkoa wa Shinyanga na hivyomiongoni mwa wilaya zilizonufaika ni pamoja na Kishapu.
“Wakati daktari anatoa taarifa hapa alisemaHospitali ya Wilaya ina changamoto gari la wagonjwa naomba niwambie wana-KishapuMheshimiwa Waziri Mkuu alinipa magari manne kwa hiyo na mimi nimegawa kwa hospitalizetu na mojawapo tutaleta Kishapu ,” alisema.
Kutokana na msaada huo wa gari hospitali hiyoitaweza kukabiliana na changamoto hiyo ambayo ilichangia wagonjwa washindwekupata huduma ya usafiri kwa haraka pindi panapokuwa na dharula.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa