Akiongea katika mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Kishapu, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi Nyabaganga Daud Taraba amesema kuwa, pamba yote iliyopo maghala ya wakulima iende katika vyama vya msingi mapema ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe 10 Septemba, 2019. Msimamo huo umekuja kutokana na utabili wa hali ya hewa kuonyesha kuwa mwanzoni wa mwezi Octoba msimu wa mvua unaweza kuanza hivyo wakulima wasio peleka pamba zao watakuwa katika hatari ya kuzipoteza. Sambamba na hayo aliwatoa hofu wakulima akiwaeleza kuwa fedha za mauzo yao ya pamba zitalipwa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa