Wanajamii wametakiwa kuwathamini na kuwatunza watu wenye ualbino kama walivyo watu wengine kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mwito huo umetolewa leo na Afisa Tarafa ya Kishapu, Giveni Noah wakati akizungumza kwenye mkutano wa mkakati juu ya watu wenye ualbino kiafya, kielimu na kiuchumi kilichofanyika leo wilayani Kishapu.
Noah ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu alisema watu wenye ualbino wanapaswa kujengewa uwezo huo ili waweze kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato zikiwemo kilimo na ufugaji.
Pia kiongozi huyo alizitaka ofisi zinazohusika kuwasaidia katika kupata mikopo ili waweze kutumia fursa kuanzisha shughuli mbalimbali kama biashara ili waweze kujiinua kiuchumi.
Kwa upande mwingine Noah alisema kuwa Serikali ya Wilaya ya Kishapu inaendelea kutoa elimu na kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ualbino ili kuhakikisha wanaishi kwa amani.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala aliahidi idara hiyo aliahidi kuwasaidia kupata mikopo ili waweze kuanzisha miradi ya maendeleo.
Pia Swalala alisema mikakati ya Halmashauri kupitia idara anayoiongoza ni kuendelea kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa watu wenye ualbino.
Awali akitoa tathmnini kuhusu watu wenye ulemavu Kishapu, Mwenyekiti wa Chma acha Watu wenye ualbino Tanzania (TAS) KIshapu, Seif Rashid alisema kuwa hali imeanza kutengemaa.
Alisema uelewa kuhusu watu wenye ulemavu umeongezeka na ameanza kuonekana kuwa ni mtu muhimu katika jamii tofauti na hapo awali na kuwa familia zao zimeanza kuwakubali na kuwatetea.
Rashid alibainisha ushirikiano baina ya Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi Wilaya ya Kishapu na TAS umeendelea kuwa imara.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa