Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho amewasisitiza wazazi kuwaandikisha watoto wao shule ili wapate elimu itakayowasaidia katika mazingira yanayowazunguka.
Kabeho alitoa kauli hiyo Agosti 20 wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2018 wilayani Kishapu wakati ukipitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema wazazi wana wajibu wa kuwasomesha watoto wao na si kuwapa majukumu ambayo yanawanyima wasaa wa kwenda shule na kupata elimu.
“Ndugu zangu wazazi hivi sasa tunatambua Serikali yetu ya Awamu ya Tano inaendelea na Mpango wa elimu bure, imefuta ada na michango iliyokuwa mzigo kwa wazazi hivyo mtumie fursa hiyo kuwasomesha watoto wenu,” alisistiza.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wananchi imewekeza katika ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo madarasa, mabweni, nyumba za walimu, mabwalo na vyoo ili elimu itolewe katika mazingira mazuri.
Alibainisha kuwa tangu mwaka 2015 hadi 2018 idadi ya wanafunzi walioanza chekechea imeongezeka kutoka 917,000 hadi milioni 1.1 huku darasa la kwanza wakifikia milioni 1.6 kutoka milioni 1.3 na darasa la kwanza ni asilimia 85.77
Alibainisha kuwa Serikali inafanya uwekezaji wa elimu imeajiri walimu wa sayansi lakini pia inatambua umuhimu wa sayansi imewekeza katika vifaa vya maabara katika shule za sekondari 1625 nchini hatua inayosaidia wanafunzi kusoma kwa vitendo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa