Kamati ya fedha, utawala na mipango katika halmashauri ya wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga imeridhishwa na kupongeza hatua ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Hayo yamejiri leo wakati ikifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/2020.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mh, Boniphace Butondo walijionea hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ambapo walifanikiwa kutembelea miradi 6 katika kata mbalimbali katika wilaya ya Kishapu.
Kati ya miradi hiyo ni pamoja na shule ya sekondari Mwataga yenye mradi wa vyumba vitatu vya madarasa. Shule ya sekondari uchunga yenye mradi wa vyumba vuwili vya madarasa. Shule ya sekondari Ukenyenge yenye mradi wa vyumba vitatu vya madarasa. Urekebishaji wa vyumba 22 vya madarasa Mwadui C. Kukamilisha ujenzi wa chumba kimoja cha maabara shule ya sekondari Mwanima, na ukamilishaji wa ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya sekondari Igaga.
Miradi hio mbali na kutekelezwa na serikali pia nguvu za wananchi zimechangia ambapo kukamilika kwa miradi hio itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na maabara kwa ajili ya elimu bora kwa njia ya vitendo.
Kamati imeipongeza serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii ambapo asilimia kubwa ya miradi hii imekamilika huku mingine ikiwa imabakiza ukamilishaji kwa asilimia ndogo.
Catherine Ngowi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa