Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wameridhishwa na maendeleo ya miradi ya elimu inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali.
Hayo yamebainika leo wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa wameambatana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya hiyo ya kukagua miradi mbalimbali.
Waliweza kukagua miradi inayoendelea kutekelezwa katika shule ya msingi Wishiteleja kata ya Mondo, Muungano kata ya Mwadui Lohumbo pamoja na Mwanima kata ya Busangwa.
Wakiwa katika ziara hiyo walipongeza Idara ya Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa ubunifu pamoja na wananchi wanaoshiriki kwa kujitolea nguvu kazi kwenye miradi mbalimbali.
Walibainisha pamoja na kuwepo kwa changamoto ndogondogo zinazokabili maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo lakini inakwenda vizuri kwa ushirikiano mkubwa wa wananchi na Serikali.
Katika shule ya msingi Muungano jumla ya sh. milioni 20 zimetumika kutekeleza mradi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu huku nyumba ya walimu ikitarajiwa kukarabatiwa endapo fedha zitapatikana.
Pia sh. milioni 60 zinatarajiwa kukamilisha mradi wa nyumba ya walimu na madarasa katika shule ya msingi Wishiteleja ambapo utakuwa mkombozi kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Kwa upande wa elimu sekondari ujenzi wa mradi wa nyumba ya walimu sita (six in one) inayojengwa katika shule ya sekondari Maganzo nao ulitembelewa na kamati hiyo ambapo kwa sasa upo katika hatua ya kupaua.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa