Kaamati ya Siasa ya wilaya ya Kishapu ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Ndg Shija Malisha Ntelezu imewapongeza wataalamu wote kwa usimamizi mzuri wa miradi inayoendelea chini ya usimamizi wa mkuu wa wilaya, Mhe. Joseph Modest Mkude
Kamati ya Siasa imewapongeza wataalamu leo tarehe 01 septemba 2022 katika ziara iliyofanya ya kukagua miradi mbalimbali inaotekelezwa katika wilaya ya Kishapu baada ya kulidhishwa na kasi ya usimamizi wa miradi inayoendelea
Akizungumza mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ndg; Shija malisha Ntelezu mbele ya Mkuu wa wilaya na wataalam wa wilaya ya Kishapu walioambatana nao katika ziara hiyo jinsi alivyofurahishwa na utendaji kazi wao wa kushirikiana katika usimamizi wa miradi
“Naomba niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa miradi, Mimi na kamati yangu tumelizika na miradi yote tuliyopita kuikagua, nazungumza kwa dhati ya moyo kabisa bila kupepesa macho kikubwa tu inatakiwa miradi hii yote mhakikishe inakamilika ndani ya muda uliowekwa lakini sina mashaka kwa kasi hii mliyonayo imani yangu itakamilika ndani ya muda pia niwaombe ushirikiano huu na umoja huu mlionao katika utekelezaji wa miradi uimalike zaidi, tukiimba wimbo mmoja kazi kwetu inakuwa rahisi sana alizungumza shija Ntelezu
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Ccm (UVCCM) Ndugu Joseph Kwilasa alimpongeza mkuu wa Wilaya pamoja na timu yake kwa ufatiliaji wa karibu wa miradi na kuhakikisha inaendana na kasi inayotakiwa
Binafsi naomba nikupongeze Mkuu wa Wilaya wewe pamoja na timu yako ya wataalamu kwa ufuatiliaji wa karibu wa miradi na mnapambana sana kuhakikisha inakamilika kwa muda unaotakiwa jitihada hizi zinaonyesha kabisa upatikanaji wa mafanikio makubwa ndani ya Wilaya yetu kikubwa ni kuendelea kufatilia kwa ukaribu licha ya changamoto ndogo ndogo ambazo huwa hazikosekani tusichoke, kwa kweli kila mradi tuliouona upo vizuri hongereni sana alizunguza kwilasa
Aidha katika ziara hiyo kamati ya Siasa imetembelea mradi wa wa maji Igaga Lagana ambao ukikamilika utahudumia vijiji 13, Ujenzi wa Jengo la Dharula hospitali ya Dr Jakaya, Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa shule ya sekondari Isoso, ukamilishaji wa Zahanati ya kiiji cha Mangu, Ukamilishaji wa Zahanati ya kijiji cha Mwamashimba, Mradi wa Barabara ya masanga-mwamalasa na mradi wa umeme Wa Rea.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa