Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kishapu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bi. Nyabaganga Taraba wamefanya ziara leo Desemba 2, 2020 ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Ziara hiyo ililenga hasa kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi zilizopo katika kata za Idukilo, Bubiki, Busangwa na Mwadui Luhumbo. Badhi ya shule hizo zilizotembelewa ni Shule ya Msingi Nyenze yenye mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu saba ya vyoo. Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu saba ya vyoo katika shule ya Msingi Idukilo. Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu pamoja na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Bubiki B. Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu nane ya vyoo katika shule ya msingi Nyasamba na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu saba ya vyoo katika shule yaMasagala.
Katika ziara hio Mkuu wa Wilaya ya Kishapu alizipongeza kamati za ujenzi za shule hizo kwa kazi nzuri iliyofanyika huku akiwaasa wale ambao bado hawaja kamilisha ujenzi kukamilisha mapema ili wanafunzi waanze kutumia miundimbinu hizo.
“Sisi sote katika nafasi zetu za kazi tunaiwakilisha serikali, hivyo unaposimamia mradi kama hii tufanye kwa ajili ya nchi yetu. Nawapongeza sana kwa kusimamia hii miradi vizuri kwani mmeonyesha ukomavu wa uzalendo kwa nchi yenu. Lakini pia natoa rai kwa hii miradi mingine ambayo haijakamilika, nawaongezea wiki moja mkabidhi mradi”. Amesema Taraba
Hata hivyo katika ziara hiyo walipendekeza kuwa kamati itafanya kikao ilikufanya tathimini ya gharama zilizotumika katika ujenzi wa mirad hiyo. Aidha fedha zilizobaki kwa baadhi ya mirad izitumike kununulia mabati na mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vingine vya ziada vya madarasa ambapo nguvu za wananchi zitatumika katika kukamilisha miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa