Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imefanya ziara katika Kituo cha Afya Kishapu leo tarehe 30 April 2020 ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hio Dr. Yudas Ndungile ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Katika kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na Homa Kali ya Mapafu aina ya virusi aina ya Corona, Kituo cha Afya Kishapu ilichaguliwa kuwa ni kituo cha Dharura kwa ajili ya wagonjwa wa corona.
Katika ziara hio kamati ya ulinzi na Usalama imeendelea kusisitia watu kufuata maelekezo wa wanayopewa na wataalamu wa Afya ikiwa ni pamoja na kujilinda binafsi dhidi ya Corona na endapo mtu amejigundua ana ugonjwa huo ni vyema kujitenga kuliko kwenda quarantine.
Pia wameshauri elimu kutolewa kwa walinzi namna sahihi ya kuopokea wagonjwa ili kuepusha kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona. Pia kuwepo na vifaa vya ulinzi na walizni wawe makini kulinda vifaa hivyo.
Aidha, miongozo inayoelezea ya dalili za awali za ugonjwa wa Corona, jinsi ya kujikinga na Corona pamoja na namna ya kuwahudumia wagonjwa isomwe kwa wahudumu wa Afya na kamati zote za maafa ni muhimu kuzijua.
Kadhalika, Mwenyekiti wa kamati hio ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa Maandalizi mazuri juu ya kukabiliana na Corona huku akisisitiza kuwepo kwa vifaa vyote vya matibabu vinavyotumiwa na madaktari viwepo tayari muda wote .
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ameiomba kamati ya ulinzi na Usalama kuzidi kuhamasisha wadau waendelee kuchangia vifaa vya matibabu ya Corona pamoja na dawa. Pia anaishukuru kamati ya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa