Shirika la world Vision limekabidhi Madawati 860 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Akikabidhi Madawati hayo Mratibu wa World Vision Wilaya ya Kishapu Bw. Yohana Masanja leo Tarehe 02 Septemba 2022 mbele ya Madiwani wa kata ambazo zitanufaika na Madawati hayo
Bw. Masanja amesema walipokea wito wa kusaidiana na Serikali kutatua Changamoto ya upungufu wa Madawati katika Wilaya ya Kishapu
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Msingi Ndugu Baraka Mwijarubi amekili kupokea Madawati 860 kutoka katika Shirika la World Vision
"Tumeshapokea Madawati 860 utoka World Vision ambayo kuanzia sasa yatasambazwa katika kata Nne ili yaanze kutumika pia tunawakaribisha na Wadau wengine karibuni ambao wapo Tayali kushirikiana na sisi kutatua Changamoto hizi za Madawati" alisema
Aidha mwenyekiti wa kamati ya Elimu ambaye ni Diwani wa kata ya Talaga Mhe. Richard Dominick Amewashukuru sana World Vision kwa Mchango wao wa Madawati 860 ambayo yatapunguza kwa Kiasi kikubwa upungufu wa Madawati katika Shule za Misingi Pia alitumia furusa hiyo Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazoendelea kuzifanya.
Picha ya Madiwani wakipokea Madawati
Picha ya Madawati
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa