Kaya 2821 za walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu zimehuisha vitambulisho vyao vya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa.
Mratibu wa TASAF wilaya hiyo, Sospeter Nyamhanga amebainisha hayo leo Aprili 08, 2019 wakati akizungumzia zoezi la uwezeshaji kaya maskini kwa kipindi cha Januari hadi Februari.
Nyamhanga alisema katika zoezi hilo ambalo sh. Milioni 244.2 zilitolewa kwa kaya 5959 kwa vijiji 78 walengwa wamehamasika na kuhuisha vitambulisho vya ambavyo vilikuwa vimekwisha muda.
”Pamoja na CHF hivi sasa kulipiwa sh. 30,000 kutoka sh. 10,000 ilivyokuwa awali walengwa wamekuwa wakilipia angalau nusu pindi wanapopata fedha kasha humalizia kiasi kilochobaki wakati wa zoezi linalofuata.
Aidha, pamoja na changamoto ndogondogo zinazojitokeza zikiwemo usafiri zoezi hilo limefanikiwa kwani walengwa wanazitumia fedha wanazpata kwa matumizi sahihi.
Mratibu huyo aliongeza kuwa kutokana na ufuatiliaji baadhi ya kaya zimeonesha mabadiliko kimaisha kwa kutumia fedha hizo kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.
Alifafanua kuwa katika kaya hizo imebainika wanufaikaji wamenunua mifugo ikiwemo mbuzi, kondoo na kuku huku wengine wakifanya biashara ndogondogo.
Pia baadhi ya walengwa tayari wamebadilisha aina za makazi yao kutoka nyumba za tembe na nyasi za awali na kuanza kujenga nyumba za kisasa za bati hali inayoleta matumaini katika miradi kama hii.
“Lengo la mpango wa TASAF siku zote ni kuziwezesha kaya maskini kujikwamua kiuchumi na ndiyo maana mara kwa mara katika zoezi hili tunatoa elimu ili kuwaelekeza namna bora kutumia fedha wanazowezeshwa,” alisema.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa