Mahakama ya wilaya Kishapu imemhukumu kifungo cha maisha Tine Christopher Mbembele.(51) mkazi wa Maganzo kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka (7)
Mbembele amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kujiridhisha na kumkuta na hatia ya kumlawiti mtoto huyo
Katika shauri namba 54 la mwaka 2021 lililowasilishwa na mwendesha mashtaka wa serikali Masenza Magunila
mshtakiwa anadaiwa kufanya kosala la kulawiti kinyume na kifungu cha sheria namba 154 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili sambamba na kifungu namba 2 kifungu kidogo cha kwanza na cha tatu kosa alilofanya katika kijiji cha Maganzo katika halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mnamo tarehe 15 -06-2021.
Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Kishapu Amada .K.Ismail amesema mahakama imemtia hatiani mshtakiwa baada ya kusililiza mashahidi wanne akiwemo shahidi namba moja ambaye ni Bibi wa mtoto, shahidi wa pili ambaye ni daktari wa Hospitali ya Kolandoto huku shahidi mwingine akitajwa kuwa ni mtoto wa mshatakiwa pamoja na askari polisi.
Hakimu Amada .k.Ismail amesema mahakama imezingatia ushahidi wa fomu ya polisi namba 3 uliotolewa na shahidi namba mbili ambaye ni daktari katika Hospitali ya Kolandoto aliyeithibitishia mahakama kuwa alipompima mtoto huyo alikuta michubuko na kueleza kuwa aliingiliwa na mwanaume nyuma ya maumbile
Uthibitisho mwingine umetolewa kwenye Taarifa ya uchunguzi wa kijamii wa awali kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Kishapu ukithibitisha Tukio la mtoto huyo kulawitiwa.
Baada ya mahakama kusililiza pande zote za ushahidi pamoja na kuthibitishiwa na vielelezo viwili kikiwemo cha fomu ya polisi namba tatu pamoja na maelezo ya onyo yaliyotolewa na mshtakiwa mwenyewe ambaye alikiri kutenda kosa hilo kwa shahidi namba nne aambaye ni askari polisi .
Akisoma hukumu hakimu Amada.k.Ismail amesema baada ya kuzingatia sheria iliyomtia hatiani mshitakiwa kwa kosa la kumlawiti binti mwenye umri chini ya miaka kumi adhabu yake ni kifungo cha maisha na hivyo mahakama imemuhukumu Tine Christopher Mbembele kifungo cha maisha jela.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa