Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kishapu Ndugu. Abednego Madole amekipongeza Sana kikundi cha Umoja ni Nguvu kilicho Kijiji cha Beledi katika Kata ya Lagana kwa kufanikiwa kurejesha Mkopo wa (4,300,000/=) Mkopo ambao walipatiwa na Halmashauri.
Pongezi hizo amezitoa leo Tarehe 13 Octoba 2023 katika Hafla fupi ya kukabidhi Ngo'mbe kwa Wanakikundi
"Hongereni Sana wanakikundi kwa hatua mliyofikia mmekuwa mfano kwa Vikundi vingine jambo la kumaliza kurejesha mkopo ni jambo kubwa Sana hii inaonyesha ni jinsi mlivyo na uwezo wa kujisimamia endeleeni kujisimamia vyema pamoja na kufata kanuni na Sheria mlizo jiwekea, Halmashauri ipo tayari kushirikiana na nyinyi kupitia ofisi ya Maendeleo ya jamii" alisema Madole
Awali akiwasilisha Taarifa kwa Mgeni Rasmi Katibu wa Kikundi cha Umoja ni Nguvu Bw. Nkuba Shija Masebo amesema kwamba kikundi kilianza na mtaji wa Shilingi 75,000/= baada ya Hapo walipata mkopo wa 4,300,000= kutoka Halmashauri mkopo huu ulisaidi kununua mbuzi 42 na hadi sasa kikundi kina mbuzi 192, Asali mbichi Lita 50 pamoja na ngo'mbe 9 ambao kila mwana kikundi amegawiwa ngo'mbe mmoja mmoja.
Aidha kikundi kilifanikiwa kurejesha mkopo wote na kubakiwa na faida ya 800,000/=
Kwa upande wake Afisa Nyuki Bw, Revocatus Lucas Mboya amesema Kwamba jambo lilifanyika kwa kikundi ni jambo kubwa Sana na nimuhimu kwa vikundi vingine kuiga
"Jambo ambalo limefanyika Tayari ni Alam tosha, jambo la kujifunza katika kikundi hiki ni nidhamu, kikundi hiki kina nidhamu kubwa pamoja na bidii katika uwajibikaji wa majukumu kwa sasa tayari mmeonyesha njia kwa wengine" alisema Mboya
"Pia kikundi hiki kinajishughulisha na ufugaji wa Nyuki na mimi kama Afisa Nyuki nitawepeni ushirikiano pamoja na kutafuta soko la uhakika kwaajili ya kuuza Asali." Aliongezea Mboya
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Beledi Ndugu. Dotto Izengo ameahidi kutoa ushirikiano kwa kikundi hicho muda wote wanapo hitaji msaada kutoka katika Serikali ya Kijiji pia amewapongeza za Sana na kubainisha faida za kila mwanakikundi ambazo wanazipata kwenye kikundi ni pamoja na kusaidia Familia zao kiuchumi, chakula na sare za shule n.k
Pia Ndugu. Madole alitumia furusa hiyo kuwahasisha wananchi waliofika eneo hilo kujiungu na Bima ya Afya CHF.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa