Mkuu wa wilaya ya kishapu mhe Joseph Modest Mkude leo 09.09.2021 amekutana na watendaji wote wa vijiji na kata pamoja na maafisa ugavi wote, katika ukumbi wa kishapu sekondari, lengo hasa ni kutafuta mbinu za kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kutokana na kilimo cha zao la pamba kwa kushirikiana na watendaji wote na maafisa ugavi katika kuhakikisha mapato yanaongezeka, kutokana na mradi wa pamba ambao ulifunguliwa ki mkoa tarehe 23.08.2021 na ki wilaya tarehe 24.08.2021 na balozi wa pamba Aggrey Deaisile Joshua Mwanri, kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilimo cha kisasa cha pamba
Mkuu wa wilaya, katika kikaoo akizungumza na wakuu wa idara na watendaji ametoa maelekezo ya kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka na wananchi wanapatiwa elimu ya kutosha kuhusu mradi wa pamba na wahakikishe angalau kila mwananchi amelima heka tatu (3) za pamba kwa kufata kanunu bora ili kuongeza tija katika zao la pamba
“naomba nitoe maeelekezo kwa wakuu wote wa idara, watendaji na maafisa ugavi hakikisheni mnaenda kujisimamia wenyewe katika ukusanyaji wa mapato kwa sababu vyanzo vya mapato tunavyo vingi sana tusilale watendaji wa kata, nyinyi ni ma boss katika kata zenu hakikisheni kwenye mageti mnakusanya mapato, muda wa usiku magendo yanapitishwa mno uzuri kishapu, tuna vijana wengi sana wa jeshi la akiba wekeni ulinzi shirikishi ili kudhibiti ukwepaji wa kulipa kodi IT hakikisha una monitor na unatolea taarifa kwa mkurugenzi”….mhe mkude alisema
“hasa katika zao la pamba tukisimamia vizuri na kuhakikisha kila mwananchi wa kishapu angalau analima heka tatu(3) za pamba, kwa kufata kanuni bora, tuna uhakika wa kuzalisha tani laki moja kwa mwaka , na uzuri mkurugenzi ameweka mfumo bora wa wanunuzi na lazima wanunue kwetu, basi naomba tuwe pamoja katika hili la ukusanyaji wa mapato” aliongezea mhe mkude
Pia mhe Joseph Mkude alitumia fursa hiyo kumshukuru mkurugenzi mtendaji (w), wakuu wote wa idara, watendaji wote na maafisa ugavi wote, kwa kuhudhuria kikao muhimu cha mapato ya wilaya, na amewaonya watendaji wote wazembe na watoro kazini, ambao hawakai ofisini na wale ambao hawasomi mapato na matumizi katika vijiji vyao kuacha tabia hiyo mara moja.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa