Na Ofisi ya Habari, Kishapu
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kupitia kwa wafadhili shirika la Investing in Children and their Society (ICS) imepongezwa kwa mradi wa kisasa wa huduma ya maji ya bomba la Ziwa Victoria kwa njia ya kielekroniki eneo la Maganzo.
Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 kitaifa, Amour Hamad Amour wakati wa kukagua na kuzindua mradi huo wenye thamani ya sh. milioni 755.
Amour alisema mradi huo utasaidia kupunguza upotevu wa maji kwni watumiaji watafanya malipo ya kabla katika kupata huduma ya maji tofauti na mfumo wa kawaida.
Alisema utaweka uwazi kwa watumiaji wa maji na kuhakikisha matumizi bora ya maji ili kuhakikisha mapato kwa wananchi kuchangia kupitia huduma ya maji.
Kiongozi huyo alifafanua kuwa hiyo itatokana na kuwa hakutakuwa na udanganyifu wa mapato na kutenda haki kuepuka matumizi mabaya ya fedha za umma kutokaa na mapato.
Alisema udanganyifu huo utaepukwa kutokana na ukweli kuwa fedha sasa hazitapita tena mikononi mwa mtu badala yake mwananchi atalipa moja kwa moja kwa njia ya kielekroniki.
Katika mradi huo mtumiaji atatakiwa kununua uniti za maji kupitia kwa wakala kwa njia ya mtandao wa simu.
Amour aliipongeza ICS na halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa mradi huo na kusema kuwa ni muhimu kwa wananchi na hivyo kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi na salama.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri na tangu tuanze mbio hizi za Mwenge wa Uhuru mwaka huu Kishapu ni mradi wa pili, tulipita Dodoma wilaya ya Chamwino tukakuta wananchi wanautumia na hii huepusha umwagikaji ovyo wa maji,” alisema.
Mradi huo wa maji ya Ziwa Victoria katika kata hiyo ya Maganzo wilayani Kishapu una jumla ya mawakala 11 na vioski 25 kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa