• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

KISHAPU YAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI

Posted on: January 12th, 2023


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ameongoza zoezi la kupanda miti 1000 ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Zoezi hilo limefanyika leo Alhamisi Januari 12, 2023 pembezoni mwa eneo la Bwawa la maji kijiji cha Kishapu likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo katibu Tawala wa Wilaya, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali Wilayani Kishapu.

Akizungumza baada ya zoezi hilo DC Mkude aliwashukuru waliojitokeza katika zoezi hilo na kutoa wito kwa wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti ikiwemo ya matunda.


"tuzitumie vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti hasusani miti ya matunda lakini pia miti hii inayotunza maji tutaendelea kupata katika Vyanzo vyote vya maji"

DC Mkude ameeleza kuwa jitihada kubwa za Serikali ambazo zinafanywa kulinda mazingira ziungwe mkono na wananchi kwani ni jukumu la kila mmoja.


Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi wote wanaozamia katika eneo hilo kwaajili ya kufanya kilimo na makazi kupisha mala moja kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu Emmanuel Johnson, amesema kuwa maeneo ya Wilaya ya Kishapu yana mvua kidogo hivyo wanategemea sana kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia mabwawa.

Ndg. Johnson Amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufufua mabwaya yaliyoharibika ili yaweze kusaidia wakulima na wafugaji.


" jitihada ambazo zinafanyika kwa sasa ni kufufua mabwawa yaliyoharibika, tumefufua Bwawa la Kiloleli, Mihama na Beledi, Kwa Mwaka huu Halmashauri imetenga Fedha kwaajili ya kufufua mabwawa zaidi kauli mbiu yetu ni kuhakikisha Wilaya yetu inakuwa na mabwawa zaidi kwaajili ya kilimo na ufugaji".

Naye Diwani wa kata ya Kishapu Joel Charles Ndettoson ameeleza kuwa Bwawa hili linahudumia zaidi ya kata Nane na Wilaya jirani ya Maswa Mkoani Simiyu.


"Bwawa hili linasaidia zaidi ya kata nane, Bwawa hili mbali na wanakijiji wanaotumia Kuna Shughuli za kimaendeleo zinazotumika eneo hili tumeona leo tupande miti zaidi ya 1000 pia tumeweka mikakati ya kusimamia Bwana hili ili liendelee kutusaidia.


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kishapu Bw Elikana Masanja amefurahishwa na ujio wa Mkuu wa Wilaya pamoja na msafara wake kwa uamzi wa kupanda miti katika eneo hilo


"Nafurahia sana kwa ujio wa Mkuu wa Wilaya katika Bwawa hili na kuamua kupanda miti katika eneo hilo kwa Sababu itasaidia sana katika utunzaji wa Vyanzo vya maji na Bwawa hili litareje katika thamani yake.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • DC MKUDE ATEMBELEA MGODI WA MWADUI KUJIONEA HATUA ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA BWAWA LA MAJI TOPE KUBOMOKA

    January 23, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPITISHA MPANGO WA BAJETISH BILIONI 39.4 KWAAJILI YA MAENDELEO

    January 20, 2023
  • KISHAPU YAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI

    January 12, 2023
  • BALOZI WA PAMBA NCHINI TANZANIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA

    January 09, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa