Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeadhimisha Sikuya Mazingira Duniani huku ikiwa imefanikiwa kufanya shughuli mbalimbali zauhifadhi mazingira ikiwa upandaji miti laki mbili.
Akiongoza maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya yaKishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba alibainisha kuwa wilaya hiyo imshiriki katikaupandaji miti, usafi wa mazingira na utunzaji vyanzo vya maji.
Mhe. Taraba alisema utunzaji wa vyanzo va majiumefanyika kwa kuzuia mifugo kulishwa kwenye maeneo ya hifadhi za misitu(ngitiri) ili kuzuia ukame kutokana na ukosefu wa mvua.
Kutokana na hilo Mkuu huyo wa Wilaya aliagizawananchi waliovamia hifadhi hizo za misitu kuondoka ifikapo mwezi Agosti mwakahuu ili kuepusha uharibifu wa mazingira.
“Tunahitaji mazingira yaliyotunzwa kwa ajili yamaisha yetu na vizazi vyetu na uharibifu wa eneo huathiri watu wengi kwaniekolojia haina mipaka. Tukiharibu mazingira tunatishia uhai wetu,” alisisitiza.
Pia aliagiza kila mwananchi atunze eneo lakelinalomzunguza kwa kufanya usafi ikiwemo kukata nyasi ndefu na kuchoma takatakahuku akisisitiza usimamizi wa sheria kutunza mazingira.
Kwa upande mwingine aliagiza kila kijiji, taasisizikiwemo shule viwe na vitalu cha miche ya miti isiyopongua 2000, Halmashaurikuwa na miche laki moja ili ipandwe na kila familia ioteshe miti isiyopungua 10.
Mhe. Taraba alizitaka shule zianzishe klabu zamazingira ili vijana wajifunze kwa vitendo huku akiwataka viongozi kuendeleakuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa