Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imezindua mradi wa Mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la IMA WORLDHEALTH, Pamoja na Chuo cha Cornel.
Lengo kuu la mradi huo ni kupunguza udumavu kwa asilimia 7 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao unatekelezwa katika halmashauri 36 zilizo ndani ya mikoa mitano ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo amefungua kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata.
Imeelezwa mradi huo utasaidia kuimarisha mikoa na halmashauri zake kwa kuzijengea uwezo wa watendaji wake wa sekta zote zinazohusika na masuala ya lishe kuhusu kupanga na kufanya ufuatiliaji wa shughuli hizo katika jamii.
Pia utachangia fedha za utekelezaji kwenye bajeti na mipango ya mkoa na halmashauri 36 kwa njia ya ruzuku ya uwajibikaji na kuhakikisha fedha zitakazotolewa hazitaifanya mamlaka hizo za Serikali zisitenge fedha kwa ajili ya masuala ya lishe.
Hivyo badala yake utahamasisha ongezeko la bajeti ya shughuli za lishe kupanda katika kipindi chote cha mradi huo unapoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa