• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KIMKOA YA FANYIKA KISHAPU

Posted on: March 8th, 2023

Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Mkoani Shinyanga, yamefanyika katika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu, huku wanawake wakitakiwa kupaza sauti za vitendo vya ukatili wa kijinsia, pamoja na kuchangamkia fursa ya Mikopo asilimia 10 kujikwamua kiuchumi.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Machi 8,2023 katika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa Serikali, Chama, huku likiendana sambamba na utoaji wa mifano ya hundi katika vikundi vya wanawake wajasiriamali na utoaji wa Gesi za kupikia.

Akizungumza Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewataka wanawake mkoani humo kuchangamkia fursa za mikopo asilimia 10 ambazo zinatolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani ili wapate shughuli za kufanya na kuinuka kiuchumi.

"Nawapongeza Wakurugenzi kwa kuendelea kutoa fedha za mikopo asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na ninaomba vikundi ambavyo vinapewa fedha hizi za mikopo vifuatiliwe ili fikie malengo na kujikwamua kichumi," amesema Mkude.

"Nawaomba pia wanawake wajasiriamali katika utengenezaji wa bidhaa zenu, muwe wabunifu na kutengeneza bidhaa zenye ubora pamoja na kuzitangaza kupitia mitandao ya kijamii ili kuongeza masoko zaidi yakiwamo ya nje," ameongeza.

Katika hatua nyingine Mkude amewataka wanawake kupinga masuala ya Mila na Desturi zenye madhara ambazo zinakandamiza wanawake kupata fursa mbalimbali ikiwamo nafasi ya uongozi.

Pia alisisitiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya kujikinga na Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, ugongwa wa COVID-19 ikiwamo kupata Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kuwapaleka wa watoto kupata Chanjo ya pili ya Surua.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake mkoani Shinyanga Dk. Regina Malima, akisoma Risala ya Wanawake kwenye maadhimisho hayo, amesema changamoto ambazo zinawakabili wanawake ni ukosefu wa Rasilimali fedha, baadhi kuwa na uelewa mdogo masuala ya ujasiriamali, kushindwa kutumia fursa zikiwano za mikopo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akisoma taarifa ya Mkoa amesema katika uwezeshaji wanawake kiuchumi kipitia fedha za mikopo kimeshatolewa kiasi cha fedha Sh.bilioni 2.5 kuanzia mwaka wa fedha 2022 hadi Machi 2023.

Aidha, Kauli Mbiu katika Maadhimisho hayo ni Ubinifu na Mabadiliko ya Teknolojia, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia, huku Maadhimisho hayo yakihudhuliwa pia na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele

Mbunge wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Christina Mzava akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Wanawake wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kimkoa wa Shinyanga yamefanyika wilayani Kishapu Kata Mwamashele

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akitoa mfano wa hudi kwa vikundi vya ujasiriamali kupitia fedha za mikopo ya halmashauri asilimia 10 ya mapato ya ndani kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA SEKE- IDIDI

    March 22, 2023
  • DC MKUDE ATOA MAELEKEZO ULIPAJI FIDIA WAHANGA WA TOPE LA MGODI WA MWADUI

    March 21, 2023
  • DC MKUDE AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAOFISA UGANI NA WATENDAJI WA KATA

    March 09, 2023
  • SHULE YA SEKONDARI BUSIYA YA PATA MSAADA WA SARUJI MIFUKO 140

    March 08, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa