Maafisa mifugo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga watakiwa kuacha tabia yakukaa ofisini na badala yake waende kwa wananchi kusimamia ukarabati na ujenzi wa majosho unaoendelea katika kata mbalimbali wilayani humo ili kuepusha tatizo la kujengwa kwa majosho yasiyokuwa na ubora.
Maagizo hayo yametolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mh. Boniphace Butondo wakati wa kikao walichoketi viongozi pamoja na wataalamu mbalimbali lengo la kufanya tathimini nakujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo mwenyekiti huyo amewaagiza maafisa mifugo katika wilaya hio kuhakikisha wanafatilia ukarabati na ujenzi wa majosho katika katambalimbali wilayani hapa. “zimetolewa fedha kwa ajili ya kuchanja mifugo , kata kama Mwamalasa walipata vifaa hivyo, tunaomba vifaa hivyo mhakikishe mnapeleka sehemu husika, simamieni ubora wa ukarabati wa majosho hayo, tusipoteze hizo fedha, majosho haya tunataka sasa yaanze kufanya kazi, dokta usikae hapa nataka hio miradi ikamilike kwa sababu awamu inayokuja tunakwenda kutembelea miradi hio ya majosho ”
Naye afisa mifugo wilayani Kishapu Bwana Alphonce Bagambabyake licha ya kuahidi kufuatilia zoezi linaliendelea la ukarabati ujenzi wa mjosho hayo, bado amewataka wanananchi kuhifadhi na kulinda miundombinu ya majosho huku akieleza kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa majosho ni mali yao pamoja na kijiji.”ile kamati ya josho ni ya kijiji na imekuwa ndani ya kijiji na ukisema kijiji kipate asilimia inakwenda kuwa biashara, josho lengo lake ka kwanza ni kwamba wakusanye pesa kwenye mifugo, wanunue dawa, wanunue maji na gharama nyingine za josho, wizara imeleta dawa kwa wilaya nzima lengo ni majosho yote yaogeshwe ”.
Na Catherine J. Ngowi
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa