Maafisa Ushirika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wametakiwa kuvifufua vyama vya ushirika ambavyo vilikuwa vimekufa.
Mwito huo umetolewa na Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo ambapo wamesema hatua hiyo itarahisisha ununuzi wa pamba kupitia akaunti za benki.
Pia wamewataka kufanya chaguzi za viongozi mbalimbali kutoka vyama hivyo kwani msimu unaokuja ni lazima ununuzi wa pamba upitie katika vyama vya msingi.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo alisema kuwa lazima vyama vifufuliwe mapema ili kuondoa usumbufu.
Butondo alisema kuwa kama vyama vikifufuliwa na kuanza kazi mapema itakuwa rahisi kwa benki kuingiza fedha kwenye akaunti kwa usalama zaidi.
Aliongeza kuwa kutokana na wakulima wengi kutokuwa na elimu ya kufungua akaunti kwa ajili ya malipo ya pamba ni vizuri wakapatiwa elimu na benki.
Itakumbukwa kuwa kwa mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu msimu wa pamba unatarajiwa kuanza mwezi Mei.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa