• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

MAFANIKIO YA KISHAPU MIAKA 61 YA UHURU

Posted on: December 7th, 2022

Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika Disemba 9, 2022 Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imetaja kupiga hatua mbalimbali za mafanikio katika utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi ikiwemo maboresho ya miundombinu ya sekta ya Afya.



Akizungumza leo Jumatano Disemba 7,2022 wakati Mdahalo wa kuzungumzia maendeleo yaliyotekelezwa na halmashauri ya Kishapu kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika,

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Swalala amesema mpaka sasa halmashauri hiyo imefanya maboresho ya miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo afya ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.


Amesema moja ya mafanikio ya kujivunia ni utekelezaji wa sera zinazolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma za kijamii kwa urahisi.


“Kutokana na sera nzuri na maendeleo ambayo yamepatikana tangu kupata uhuru miundombinu sasa imeelekezwa iwe rafiki kwa wananchi wote wakiwemo wenye ulemavu, lakini tunaweza kwenda mbali zaidi kwamba kutokana na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi makundi ya watu wenye mahitaji maalumu wameendelea kuwezeshwa kiuchumi”, amesema Swalala.


“Halmashauri ya Kishapu tumeendelea kuzingatia wananchi wote wanapata huduma zote muhimu ikiwemo huduma za afya pamoja na huduma ya maji bila kutembea umbali mrefu, hayo ndio maendeleo ambayo tumeendelea kuyatekeleza”, amesema Swalala.


Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Raymond Tibakya wa Hospitali Wilaya ya Kishapu inayotambulika kwa jina la Dr. Jakaya Kikwete amesema katika kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru, serikali imeboresha huduma za afya hususani kwa akina mama wajawazito na hivyo kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.


“Hali ya utoaji huduma kwa sasa ikilinganishwa na zamani kuna mabadiliko makubwa sana itukianza na huduma za mama na mtoto zimeboreshwa sana, mwanzo huduma za upasuaji zilikuwa hazipo lakini kwa sasa zinapatikana” ,amesema Dr. Tibakya.


“Kwa sasa hospitali yetu imejengewa majengo mapya ambapo serikali kuu iliweza kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa majengo matano jengo la idara ya dharura, wodi ya watoto, wodi ya kinamama, jengo la maabara pamoja na jengo la mionzi” ,amesema Dr. Tibakya.


Nao baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kishapu wamepongeza juhudi mbalimbali za maendeleo zinazoendelea kutekelezwa na serikali kuelekea Miaka 61 ya uhuru hali ambayo imesaidia kupunguza changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaikumba jamii na kwamba wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo.


Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika, Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa kushirikiana na wananchi imeanza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii michezo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo Disemba 9, 2022.

Mwonekano wa Jengo la Mionzi katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu Muonekano wa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu Dr. Raymond Tibakya akizungumza maboresho yaliyofanyika katika huduma za kiafya katika hospitali hiyo Muonekano wa nje wa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu Mkazi wa Wilaya ya Kishapu akizungumza kuelekea maadhimisho ya Miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika Mkazi wa Wilaya ya Kishapu akizungumza kuelekea maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika Picha ya pamoja baada ya Mdahalo wa kuzungumzia maendeleo yaliyotekelezwa na halmashauri ya Kishapu kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • DC MKUDE ATEMBELEA MGODI WA MWADUI KUJIONEA HATUA ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA BWAWA LA MAJI TOPE KUBOMOKA

    January 23, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPITISHA MPANGO WA BAJETISH BILIONI 39.4 KWAAJILI YA MAENDELEO

    January 20, 2023
  • KISHAPU YAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI

    January 12, 2023
  • BALOZI WA PAMBA NCHINI TANZANIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA

    January 09, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa