Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa kushirikiana na shirika la Relief for Development Society (REDESO) imezindua mradi wa mafunzo yakutengeneza majiko sanifu kwa ajili ya kustahimili mabadiliko ya tabia ya nchi vijijini.
mafunzo haya yametolewa katika wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga ikihusisha wawakilishi 40 kutoka katika vijiji 4 ambvyo ni Muguda, Kiloleli, Beledi, Mihama.
Mafunzo haya yalilenga zaidi uhamasishaji wa ujenzi wa majiko sanifu na utumiaji wake majumbani ili kuimarisha na kulinda mazingira, kupunguza matatizo ya kiafya kwa watumiaji, kuwezesha jamii kuelewa malighafi na vifaa mbalimbali vinavyotumika kujengea majiko sanifu ili kuelimisha jamii juu ya majiko sanifu.
Afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Martin Ndamo wakati wa kufungua mafunzo hayo aliwataka wawakilishi kuwa makini wakati wa mafunzo ili wakatoe elimu kwa jamii juu ya utengenezaji, matumizi na umuhimu wa majiko sanifu kwa wanajamii katika vijiji vyao.
Naye Elizabeth Pamphil ambaye ni Afisa Mradi REDESO wakati wa mafunzo hayo alitoa elimu juu ya majiko sanifu ni banifu katika kutumia kuni au mkaa kwa kiasi kidogo katika kutoa nishati ya kupikia chakula kwa faida ya kulinda mazingira na misitu. Aina hizo ni pamoja na jiko mkombozi, jiko okoa, jiko duma na jiko chaga.
Kati ya majiko hayo, jiko okoa ni jiko ambalo limechaguliwa na mradi kwa kuwa ni rafiki zaidi kwa wanajamii, mazingira, kiuchumi, kiufanisi, kijinsia na afya kwa watumiaji.
Aidha mtaalamu wa majiko sanifu, Mwalimu Nyapi alitoa mafunzo juu ya vifaa na ujenzi wa majiko sanifu pamoja na jinsi ya kutengeneza majiko sanifu aina ya okoa. Ambapo wawakilishi waliopata mafunzo watakuwa wataalamu katika vijiji vyao na kuwawezesha kujikwamua kuichumi kupitia mradi huu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa