Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Sophia Mjema apiga marufuku kwa wafanya biashara wa vifaa vya ujenzi wanaopandisha bei za vifaa vya ujenzi bila mpangilio ikiwemo Nondo, Saruji na Mabati.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wilayani Kishapu akiwa kwenye ziara ya kikazi alipowatembelea wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi wilayani Kishapu na kuwataka waache mara moja tabia ya kupandisha bei za vifaa kwa sababu ambazo siyo za msingi, badala yake wamuunge mkono Mhe, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kukamilisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Nawaomba tuache tabia ya kupandisha bei za vifaa vya ujenzi, wafanya biashara wengi baada ya kuona miradi ya mheshimiwa Rais ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mmeona ni furusa kwenu kupandisha bei bila sababu, hamuoni kama mnakwamisha malengo ya Rais ya kukamilisha ujenzi wa madarasa hivyo basi, tumuungeni mkono Mhe, Rais, tushirikiane kwa pamoja katika kufanikisha ujenzi.
Baada ya kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wafanyabiasha wameaahidi kutoa ushirikiano kwa serikali na kukubali kuuza vifaa vya ujenzi kwa bei elekezi bila kupandisha ili kusaidiana kukamilisha miradi ya maendeleo ambayo kufikia Disemba 2021 iwe imeshakamilika.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa