Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe, Joseph Modest Mkude. Amepiga Marufuku kwa watu wanaopiga lamri Chonganishi (Lambalamba) kuendelea na Shughuli zao wilayani Humo.
Mhe, Mkude amewataka Viongozi wote wa Ngazi mbalimbali Kushirikiana na kuhakikisha wanakomesha swala la Lambalamba ambalo linaleta uvunjifu wa Amani katika Wilaya hiyo
Mhe, Mkude ameyasema hayo leo Tarehe 27 Juni 2022 katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya WIlaya ya Kishapu,
"Ndugu zangu nawasalimu kwa Jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA? Nimepokea taarifa ya uwepo wa watu hawa wanaojiita LAMBALAMBA hapa wilayani kwetu. Nitoe wito kwamba jambo hili halikubaliki katika Wilaya hii na linalalamikiwa sana na watu hasa wazee na kaya ambazo hazina kipato ni kweli kwamba watu aina hiyo ni MATAPELI na wachonganishi wanaotufanya tusiishi kwa amani tena ndani ya wilaya yetu,
Watu hao hawakubaliki na mtu yoyote na hawajapata kibali cha mtu yoyote yule toka mahali popote. Kama kuna mtu anauhakika wana vibali amlete ofisi ya Mkuu wa wilaya mara moja ili aweze kuruhusiwa kuendelea na shughuli hiyo anayotaka kuifanya. Kwa wito huu ndugu viongozi wote katika ngazi mbalimbali ninaomba ushirikiano mkubwa ili tuwabaini watu hao na kutowakaribisha kufanya shughuli zao hizo potofu, Natoa wito kwa Uongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji hakikisheni mnatoa taarifa haraka juu ya uwepo wa watu hao ili hatua za Kisheria zichukuliwe" Alisema Mhe, Mkude
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa