Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,Mhe. Boniphace Butondo ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za miradi kwa wakati.
Mhe. Butondo ametoa shukurani hizo leo Machi 28,2019 wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za kataza robo ya pili mwa 2018/2019.
Katika kikao hicho kilichohusisha pia wakuu waidara alisema kuwa wananchi wanapata huduma bora kutokana na Serikali kupelekafedha inazotenga kwa wakati.
Aidha, Mhe. Butondo ambaye pia ni diwani wa Kata yaLagana aliwataka madiwani kusimamia miradi katika kata zao na kuhakikishainatekelezwa kwa wakati.
“Madiwani tunakwenda kusimamia kata zetu katikamiradi mbalimbali kwani Serikali inatoa fedha nyingi ili wananchi wetu wapatehuduma bora hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunakamilisha miradi hiyo,”alisisitiza.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa