Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Sekondari kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Ndugu Benjamin N. Oganga ametembelea Shule ya Sekondari Mwadui Technical leo Novemba 9, 2020 alipokuwa anakagua ukarabati wa majengo pamoja na ujenzi wa mabweni na vyunba viwili vya madarasa ya shule hiyo.
Shule hiyo iliyopo katika Wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga ilianzishwa mwaka 1997 chini ya Mgodi wa Almasi wa Williamson yenye jumla ya wanafunzi 827 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne huku wanafunzi wa kike wakiwa ni 437 na wakiume 390. Fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi 226,856,239.82/= kwa ajili ya ukarabati wa majengo, Shilingi 80,000,000.00/= kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi, Shilingi 40,000,000.00/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Mkuu wa shule hiyo Ndugu Shija Dominic Kulewa ameishukuru serikali na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo huku akiahidi kusimamia ukarahati na kukamilisha ujenzi huo.
“Nashukuru sana kwa ajili ya huu ukarabati kwani majengo ya shule hii yalikuwa yamechakaa sana, kitokana na nyufa zilizokuwepo katika madarasa ilikuwa inapelekea wanafunzi kukaa darasani kwa wasiwasi sana. Hivyo natoa pongezi za dhati kwa serikali yetu kwa kuipa elimu kipaumbele “ alisema Kulewa.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu sekondari Ndugu Oganga amepongeza maendeleo ya ujenzi huo huku akiwataka kusimamia kwa umakini ujenzi huo ili majengo yawe imara huku akishauri fedha zinazibaki zitumike kupaka rangi na kuweka bati mpya kwenye majengo mengine.
“nataka mwenge ujao utakapopita hapa pawe mfano kwa maana ya ubora wa majengo. Pia fedha zitakazobaki kutokana na ujenzi huu zitumike kukupaka rangi majengo mengine ili yawe ya kufanana na haya yaliyorekebishwa “ alisema Oganga.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa