MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo, kushiriki kikamilifu siku ya kuhesabiwa Sensa na watu na makazi ambayo itafanyika Agosti 23 mwaka huu.
Mjema amebainisha hayo leo Agosti 12, 2022 wakati akihamasisha wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi siku ya kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi,
Amesema zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi ni la muhimu kwa kila Mtanzania,kwa sababu Serikali itapata idadi ya watu wake kamili na kuwa virahisi kutoa huduma kwao za maendeleo kwa uwiano sawa na kujitosheleza.
“Nawaomba wananchi wa Shinyanga mshiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Agost 23 mwaka huu, ili lifanikiwe na kuirahisishia Serikali kuwa na mipango mizuri ya maendeleo kwa wananchi wake na kuwapelekea huduma stahiki,”amesema Mjema.
Aidha, amewatoa wasiwasi wananchi kuwa zoezi hilo la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi hali husiani na tozo ya kodi ya kichwa, na kuwaonya watu ambao wamekuwa wakipotosha waache mara moja sababu hawana nia njema na Taifa kusonga mbele kimaendeleo.
Katika hatua nyingine Mjema, amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, kuwa siku ya Agost 14 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye Mbio za Shinyanga Madini Marathon na uzinduzi wa kipindi cha Thamani ya Madini, matukio ambayo yamelenga kuutangaza Mkoa wa Shinyanga.
Nao viongozi wa dini waliohudhuria kwenye hamasa hiyo ya Sensa, wamempongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu wake, na kuahidi kumuunga mkono kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kuhesabiwa Sensa kupitia madhabahu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa