MKUU WA MKOA WA SHINYANGA APIGA MARUFUKU WATOTO KWENDA MINADANI.
Hayo yamejiri leo terehe 09 April 2020 katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainabu Terack alipokuwa anafanya tathimini ya kukabiliana na ugonjwa wa corona katika mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.
Katika ziara hio Mkuu wa Mkoa aliwaasa wazazi kuwa makini na watoto wao kwa kuwakataza kwenda mnadani hasa kipindi hiki cha ugonjwa wa corona, aidha waliwataka watoto kubaki majumbani ili wabaki salama.
“hatutaki watoto kwenye minada wote wabaki nyumbani, mtoto yoyote atayekuja naomba arudishasiingie mnadani”
Aidha aliwataka wafanya biashara hasa wa mifugo wanaosafiri mikoa mbalimbali kutumia sanitizers na kunawa mikono mara kwa mara pia wanunuzi wengine kununua vitu na kurudi majumbani, tusishinde mnadani bila sababu maalumu.
“Nawaomba wafanya biashara hasa wa ng’ombe mnaonunua mifugo hapa na kupeleka mikoa mbalimbali, kila mtu awe na sanitizers, pia gari unayosafiri nayo hakikisha iko salama, tulinde uhai wetu”
Kadhalika katika kukabiliana na ugonjwa wa corona tunapaswa hujikinga kwa kuepuka kwenda sehemu zenye msongamano wa watu pia kuepuka safari zisizokuwa na ulazima. Kwa takwimu iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu kuwa idadi ya vifo hadi sasa kwa Tanzania imefikia 32. Hivyo tuzidi kuchukua tahadhari kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa