Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe, Sophia Mjema ametoa sababu za mfumuko wa wa bei wa vitu mbalimbali Mkoani Shinyanga na nchi nzima kwa ujumla Mhe Mjema amezitoa sababu hizo leo Juni 14, 2022 wakati akizungumza na wananchi Wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu kkatika Ziara yake yake kikazi wilayani humo.
Amesema sababu kubwa mbili ambazo zimechangia kupanda kwa vitu mbalimbali yakiwepo mafuta na unga wa ngano ni vita kati ya Mataifa mawili makubwa Urusi na Ukrine pamoja na Ugonjwa wa virusi vya CORONA.
“Walipoanza kupigana Vita Urusi akafunga gesi yake ile gesi Urusi anazisambazia nchi za Ulaya na Nchi za Ulaya wana viwanda vingi ambavyo vinatoa bidhaa mbalimbali, zikiwepo bidhaa za ujenzi , bidhaa za chakula n.k sasa Urusi alipo funga gesi yake wale watu wa Ulaya hawakuwa na njia nyingine ya kutumia badala ya gesi kutumia walianza kutumia mafuta, gesi waliyokuwa wanaitumia bei ilikuwa chini kuliko mafuta, sasa walipoanza kutumia mafuta bidhaa lazima zitapanda bei. Manaake zile bidhaa zitoke ulaya mpaka bandari ya Dar es salaam zitoke, Dar es salaam mpaka Shinyanga lazima bidhaa zipande bei
Pia Mhe Mjema aliongezea kwa kusema sababu nyingine iliyochangia kupanda kwa bidhaa ni Ugonjwa wa CORONA
"Tukumbuke hapo nyuma mpaka leo kulikuwa na Uviko 2019 wenzetu wa Ulaya walijifungia ndani walipojifungia ndani uzalishaji ulipunguwa, uzalishaji ulipo pungua bidhaa zikapanda bei hizo ndiyo sababu kubwa mbili."
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa