Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewakumbusha Watumishi juu ya wajibu wao katika uwajibikaji wa kweli kwenye majukumu yao ili kuleta maendeleo yenye tija Serikalini.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo 01.05.2023 akiwa Mgeni Rasmi katika sherehe za Maadhimisho ya Mei Mosi ambayo ki Mkoa, yamefanyika katika Uwanja wa Mwadui, Wilaya ya Kishapu yakiwa na KAULI MBIU: Mishahara Bora na Ajira za staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi. Wakati ni sasa.
Aidha amewakumbusha juu ya kulinda Maadili ya kitanzania, ambapo amewaeleza kuwa Tanzania kama Nchi tuna maadili na tamaduni zetu tulizorithi kutoka kwa mababu zetu na viongozi wetu huku akiwataarifu kuwa Mkoa wa Shinyanga umeanzisha Kampeni ijulikanayo kama DON'T TOUCH ME, HAPA NI KWANGU ambayo inalenga kuwaelimisha watu wote na kwamba elimu hii iende mpaka kwa familia.
" Wakati tunasherehekea Maadhimisho haya, pamoja na kuipongeza sana Serikali yetu lakini tujiandae kuipokea Kampeni hii ambapo itakwenda mpaka ngazi ya familia ambapo tuwafundishe watoto na tunaowalea kukataa kabisa tabia zote zisizokuwa na maadili na wawe tayari kusema DON'T TOUCH ME, HAPA NI KWANGU pia mkumbuke uwajibikaji na maadili yetu pamoja na kuthamini Ulinzi na Usalama ambapo wenyeviti wetu wasiruhusu mtu kuingia maeneo yao kama hajulikani na ikitokea watoe taarifa kwa Mamlaka za Usalama," alisema Mhe. Mndeme.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa