Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya wamefanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda cha mataruma ya reli ya kisasa ya SGR, sehemu ya Mwanza-Isaka (KM 341) kinachojengwa Seke Ididi wilayani Kishapu.
Mhe. Mkude amesema lengo la ziara hiyo ni kufanya ukaguzi katika sehemu za kuhifadhia vifaa vya ujenzi pamoja na mafuta kutokana na matukio ya wizi ambayo yanaendelea katika mradi wa SGR.
“Tulikuwa tukipata ripoti za mara kwa mara juu ya matukio ya wizi wa vifaa vya ujenzi kama vile Saruji, nondo na mafuta kwa wingi sana, sasa tukaona tufatilie ili tubaini kama kuna mapungufu ili tuweze kushauri yarekebishwe,” alisema Mkude.
Pia Mhe. Mkude amekiri kuwepo kwa mapungufu makubwa kwenye baadhi ya maeneo ya stoo katika mradi wa ujenzi wa reli ya SGR ikiwemo kutokuelewana kwa lugha kati ya Wachina na vibarua.
Aidha, Mhe. Mkude ametoa wito kwa wananchi wote kuwa wazalendo kwa nchi yao na hasa katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama hiyo pamoja na kutoa ushirikiano ili kubaini waharifu wanao hujumu miradi na kukwamisha kukamilika kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa