Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeanzisha mnada wa Kalitu ikiwa ni njia yakujikwamua na kukuza pato lake la ndani. Mnada huo ambao upo katika kata ya Ngofila wilayani Kishapu kunafanyika shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile uuzaji wa mifugo, mazao, vyakula, vinywaji, nguo, urembo nk.
Kamati ya CMT ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imefanya ziara katika eneo hilo leo tarehe 03 Novemba 2020 ili kubaini changamoto zinazoukabili mnada huo na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuboresha baadhi ya huduma zinaozotolewa hapo. Kamati hio iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndugu Sostenes Mbwilo wamebaini kuwa licha ya mnada wa Kalitu kuwa bado ni mpya tofauti na minada Mingine bado unapiga hatua nzuri za kimaendeleo kwani shughuli mbalimbali zinaendelea.
Aidha, katika majadiliano na wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa mnada huo, Bwana Ligi Jipolo ambaye ni mwenyekiti wa mnada kwa niaba ya wengine aliomba Halmashauri kutoa ushirikiano wa karibu kwa kuwasaidia kujenga barabara ambayo ni rafiki hasa msimu wa masika, kuimarisha ulinzi siku za mnada ili kuwahamasisha wafanya biashara wakubwa kuja kwa wingi vile vile wakazi wa maeneo hayo wameishukuru Halmashauri kuwasogezea huduma hio katika makazi yao kwani inawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kadhalika, Dr. Sabinus Chaula ambaye ni Kaimu Afisa mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu aliahidi kuyafanyia kazi huku akiwashauri wafanyabiashara hao kuongeza idadi ya mifugo kwa wingi ili kuwavuta wanunuzi huku akiwashauri kujenga mabanda imara ya biashara kufuatia msimu ujao wa mvua za masika.
Katika zoezi hilo wafugaji na wafanya biashara hao wameombwa kuwa wavumilivu kwani mnada huo bado ni mpya hivyo wao ndio watakaochangia kwa asilimia kubwa kukua kwa mnada huo.
Mnada wa Kalitu ni miongoni mwa minada ya wilaya ya Kishapu huku mingine ikiwa ni Mhunze, Magalata, Nyasamba, Seke Ididi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa