Na Ofisi ya Habari Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba ameagiza uchunguzi ufanyike mara moja kubaini chanzo cha moto ulioteketeza bweni la wasichana shule ya sekondari Bunambiyu.
Tukio hilo lilitokea leo Jumatatu saa 2 asubuhi wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani na kusababisha uharibifu wa vifaa vikiwemo vitanda 12, magodoro 36 na mali zao zote.
Taraba pia amewataka wanafunzi katika shule hiyo iliyopo kata ya Bunambiyu kutoa ushirikiano wa kawaida uchunguzi ukiendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha moto huo
Kwa mujibu wa mwalimu wa shule hiyo, Lameck Manumbu pamoja na jitihada za wanafunzi na wanakijiji wa Bunambiyu kuzima moto huo hawakufanikiwa kwani ulikuwa umeshika kasi na kuteketeza bweni hilo linalotumiwa na wanafunzi wa kike 26.
Taraba akiwa katika eneo la tukio akiambatana na Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na wataalamu wa sekta mbali mbalimbali walifanya tathimini ya awali na misaada kwa wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya na timu yake waliungana na Uongozi wa Shule, Ungozi wa Kata na Kijiji na wananchi majirani na shule na walifanya kikao cha kazi kutafuta chanzo cha moto na kutafakari hatua za haraka za kuchukua.
Kwa kushirikiana na uongozi wa shule walianisha mahitaji ya haraka kuwasaidia waathirika na kuwapatia makazi ya muda huku hatua za kuwanunulia shuka zote pamoja na baadhi ya mahitaji zilifanyika.
Mkuu wa wilaya alihamasisha mchango wa papo ambapo zilipatikana jumla ya sh. 272,000 ambazo walipewa waathirika na kila mmoja alipata 10,000 kwa ajili ya mahitaji ya haraka wakati wakisubiri mahitaji mengine ya awaida ili waendelee na masomo wakati wakiwasiliana na wazazi wao.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa