Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yamefanyika leo tarehe 27 Novemba 2020 kiwilaya katika kata ya Nyasamba iliyopo katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga. Hii ikiwa ni agizo la kila wilaya mkoani Shinyanga kufanya maadhimisho hayo kabla ya tarehe 01 Desemba 2020 ili kupisha maadhimisho hayo kimkoa ambayo yatafanyika katika Halmashauri ya Ushetu.
Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu ya “Mshikamano wa Kitaifa, Tuwajibike kwa Pamoja” yalilenga hasa uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa wananchi pamoja na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi. Sambamba na hilo zoezi la ugawaji wa kondomu lilifanyika ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Aidha Katika maadhimisho hayo, shirika la THPS (Tanzania Health Promotion support) lenye mradi wa kupambana na kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa makundi hatarishi.
Mratibu wa kudhibiti Ukimwi katika halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu Abednego Madole amewataka wananchi kwa pamoja kushikamana kupambana dhidi ya maambukizi ya Ukimwi kwa kujua afya zao mara kwa mara na kuwa waaminifu katika mahusiano yao. Aidha kwa niaba ya Halmashauri alilishukuru shirika la THPS kwa ushirikiano wao katika kufanikisha maadhimisho hayo huku akiwaomba wadau wengine kupitia mkoa kuja katika Wilaya ya Kishapu ili kusaidia mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Takwimu za Ukimwi kwa miezi mitatu iliyopita ya August hadi Oktoba kutoka katika ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Jakaya Mrisho Kikwete zinaonyesha jumla ya idadi ya watu waliopima VVU katika Wilaya ya Kishapu ni 10,856. Kati ya hao wanaume wakiwa ni 4672 na wanawake ni 6184. waliogundulika kuwa na maambukizi ya VVU wanaume wakiwa ni 117 na wanawake ni 116 ambapo ni sawa na 2.1%.
“Dhana ya Kufanya maadhimisho haya kila mwaka ni kufanya tathimini ili kujua ni kwa kiasi gani janga hili limethibitiwa pia kuja na mikakati mingine ili kuendelea kupambana na janga la Ukimwi. Aidha tunaendelea kukumbushana kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa huu ili kuweza kujikinga”
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa