Serikali imewaagiza viongozi wa ngazi ya tarafa, katana vijiji kuhakiksha wanajenga mazingira ya kuwalinda watoto wawapo shulenipamoja na majumbani.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya yaKishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na AfisaTawala, Juvenary Byekwasho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrikakiwilaya yaliyofanyika kijiji cha Mwamashele.
Mhe. Taraba pia aliwaomba wazazi kushirikiana na Serikalikatika jitihada zake za kuzuia vitendo viovu vinavyofanywa kwa watoto ambavyovinawanyima haki ya kupata elimu.
Aliitaka jamii kushirikiana bega kwa bega na Serikalikatika hatua ya kuwekeza kwa watoto ambao ndio watakaoliendeleza Taifa laTanzania.
Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa ni muhimu kujengamisingi imara ya kuelekea uchumi wa viwanda kwa watoto na hilo lifanyike piakwa kuhusisha watoto ili kuwajenga.
Alikemea tabia ya baadhi ya wazazi ya kutotoaushirikiano kwa vyombo vya dola kuhusu wahusika wanaotuhumiwa kuwapa ujauzitowanafunzi na kushindwa kuendelea na masomo.
“Familia ni chanzo za ulinzi wa mtoto halafu jamiina Serikali hivyo wazazi watoe ushirikiano katika kutokomeza vitendo vinavyowasababishawatoto wapate matatizo.
“Watoto nao wasinyamaze wanapona wanatendewavitendo vya unyanyasaji watoe taarifa kwenye vyono husika ili wahusikawachukuliwe hatua,” alisema Mhe. Taraba.
Maadhimisho hayo pia yaliambatana na utoaji zawadikwa wanafunzi waliofanya vizuri kutoka shule za msingi na sekondari kwenye kataya Mwamashele sambamba na burudani kutoka kwa watoto.
Pia yalishirikisha wadau mbalimbali yakiwemomashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya OPE, Save the Children, Redeso na TCRSambayo kwa namna moja ama nyingine yanatetea haki za motto.
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Juni 16 kutambuathamani, utu na umuhimu wa motto katika jamii duniani kote ambapo kwa mwaka huukaulimbiu ni ‘Katika uchumi wa viwanda watoto wasiachwe nyuma’.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa