Mwenge wa uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kishapu, huku wananchi wakihimizwa kutunza Mazingira pamoja na vyanzo vya maji.
Kauli mbiu ya mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu (2023) inasema' Tunza Mazingira,Okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe Hai kwa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Josephe Modest Mkude kwa ajili ya kuukimbiza wilayani Kishapu na kuipitia Miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzinduliwa, mara baada ya kumaliza kuupokea kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk,Yahaya Nawanda.
Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Shinyanga, umeanza kukimbizwa leo wilayani Kishapu kwa umbali wa kilomita 118 pamoja na kuifikia Miradi Sita yenye thamani ya Sh.bilioni 1.3.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, amesema ameridhika na miradi hiyo ya maendeleo wilayani Kishapu, na yote ameizindua hakuna hata mmoja ambao umekataliwa, huku akiwataka wananchi watunze mazingira na vyanzo vya maji.
"Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, na leo nimeikagua na kuizindua tumpongeze sana Rais wetu,"amesema Karim.
Aidha, akiwa katika upanuzi wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria wa Maganzo- Masagala, amesema mradi huo ni muhimu sana katika kutatua Changamoto ya wananchi kufuata maji safi na salama umbali mrefu pamoja na kumtua ndoo kichwani Mwanamke.
Naye Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi jimboni humo na kutekelezwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwamo hiyo ya Maji.
Miradi ya maendeleo ambayo imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kuwa ni Barabara ya Buganika- Kabila Kilomita 11, vyumba viwili vya Madarasa na vyoo Sita katika shule ya Msingi ya Awali Idukilo.
Miradi mingine ni Kituo cha Afya Negezi, Mradi wa Maji Maganzo- Masagala, Mradi wa kuhifadhi Mazingira na vyanzo vya Maji katika Bwawa la Songwa, Klabu ya wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Maganzo na kuweka jiwe la Msingi Stendi ya Maganzo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa