Mwenge wa Uhuru umekimbizwa wilayani Kishapu Agosti 201, 2018 ambapo umekagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya sh. bilioni 2.2.
Katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru sehemu ya miradi iliyowekwa mawe ya msingi ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Songwa uliofadhiliwa na Serikali Kuu kupitia mpango wa kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ukiwa na thamani ya sh. milioni 400.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Charles Kabeho, mradi huo unatarajiwa kukamilika baada ya wiki mbili na unatarajiwa kuhudumia wananchi 21,500 wa eneo hilo na vijiji jirani.
Mradi mwingine ni wa ujenzi wa maji ya bomba wa Ziwa Victoria katika kijiji cha Unyanyembe uliofadhiliwa na Serikali Kuu kupitia Programu ya WSDP II ukiwa na thamani ya sh. 453 ambapo unatarajiwa
Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi Oktoba, 2017 na unatarajia kukamilika Septemba huku na kuhudumia wananchi 3,088 wa kijiji hicho na vijiji jirani huku lengo likiwa ni kutoa huduma ya maji safi na salama.
Mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, nyumba ya watumishi wawili (2 in 1) na matundu 14 ya vyoo shule ya msingi Wishiteleja kwa ufadhili wa Serikali Kuu kupitia Mpango wa Lipa kwa Matokeo (P4R) wenye thamani ya sh. 66,600,000.
Lengo la mradi ni kuboresha maisha ya watumishi na usafi wa mazingira shuleni kwa gharama za sh. milioni 66,600,000 na unatarajia kunufaisha wanafunzi, walimu na Wananchi wa kijiji cha Wishiteleja na vijiji jirani.
Mradi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi sita (6 in 1) na vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari Maganzo uliofadhiliwa na Serikali Kuu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wenye thamani ya sh. milioni 141 umefunguliwa.
Lengo la mradi ni kupunguza msongamano wa wanafu nzi darasani, kuboresha maisha ya walimu (mtumishi). GHARAMA huku ukitarajiwa kuwanufaisha wanafunzi, walimu na Wananchi wa kijiji cha Maganzo na vijiji jirani.
Mradi wa mwingine ni utengenezaji wa madawati 5,000 uliofadhiliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia mapato ya ndani ukiwa na thamani ya sh. milioni 289.3 umeonwa.
Lengo la mradi huo ni kuondoa changamoto ya upungufu wa madawati shuleni ambao umesababishwa na mwitiko mkubwa wa wazazi kuandisha watoto wao kutokana na Mpango wa Elimu bila Malipo.
Miradi ya wananchi ni pamoja na ule wa unenepeshaji wa ng’ombe wa mjasiriamali Eliudi Urassa katika Kijiji cha Ukenyenge wenye thamani ya sh. 285 na ule wa kiwanda cha mjasiriamali Mabela Masolwa wa kuweka thamani mazao ya kilimo wenye thamani ya sh milioni 555.8 umezinduliwa.
Aidha, mradi wanawake na walemavu kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani mwaka wa fedha 2018/19 wenye thamani ya sh.milioni 19.2 umekabidhiwa ambapo wanawake ni sh. milioni 12. 8 kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali na walemavu ni sh. milioni 6.4 kwa ajili ya mradi wa maji safi na salama.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa