Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wataalamu wa kilimo kote nchini kuhamia mashambani ili kutoa elimukwa wakulima.
Ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya siku mojawilayani Kishapu ambapo alizungumza na wakulima, wanachama wa vyama vya msingina wataalamu wa kilimo kutoka wilayani humo.
Mhe. Bashungwa alisema kuwa wataalamu wa kilimowakimemo kutoka Bodi ya Pamba na kuwasikiliza wakulima ili kubaini changamotozinazowakabili na kuzitatua.
Alizitaka idara zinazoshughulikia sekta ya kilimokukaa na kuandaa mpango kazi wa kutoa elimu ya kilimo chenye tija kwa wakulimawa pamba.
“Wataalamu kutoka TPRI (Taasisi ya Viuatilifu),Bodi ya Pamba kuhakikisha mikoa 17 na wilaya 56 zinazolima pamba msimamiemhakikishe wataalamu wa kilimo wanahamia mashambani wawape elimu wakulima,”alisisitiza Naibu Waziri.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa