• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

RC MNDEME AIPONGEZA HALMASHAURI KWA KUPATA HATI SAFI

Posted on: June 23rd, 2023

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu leo Tarehe 23 Juni 2023 limefanya Mkutano Maalumu wa kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.


Awali Mweka Hazina wa Halmashauri Ndugu. Georgy Sulumbwe alitoa taarifa fupi juu ya hoja zinazoikabili Halmashauri ambayo alieleza kuwa katika ukaguzi wa 2021/2022 Halmashauri ilitunukiwa hati safi ikiwa na jumla ya hoja 54 kati ya hizo 22 zimefungwa na 32 zipo katika hatua ya utekelezaji


Katika Baraza hilo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia  taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) zinazoonesha alikagua hesabu za Serikali za Halmashauri na kutoa  Hati safi ya ukaguzi.

“Mhe. Mwenyekiti nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye ametupa kibali cha kuwa mahali hapa, Mhe, Mwenyekiti nitumie furusa hii kuwapongeza kwa kupata Hati Safi katika taarifa ya CAG tunayoijadili leo nyinyi mko safi rai yangu kwenu muendelee kupata hata hii safi mwisho wa ukaguzi huu ni mwanzo wa ukaguzi mwingine msipate hati ya mashaka au hati chafu, haya mazuri mnayoyapa ni kwaajili ya ushirikiano mzuri mlionao kati ya Madiwani na Wataalamu ushirikiano huu uendelee.” Alisema Mndeme


Pia ameitaka Halmashauri iongeze kasi ya ukusanyaji Mapato kwa siku hizi Saba zilizobakia kabla ya kufunga Mwaka wa Fedha 2022/2023 ili kufikia lengo la Asilimia 100 ya Ukusanyaji wa Mapato

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson Amemwahidi Mkuu wa Mkoa kutekeleza Maagizo na Maelekezo yote yaliyotolewa kuanzia kwenye kamati ya Fedha, Kamati ya Ukaguzi

“Mhe. Mwenyekiti nichukue furusa hii kwanza nishukuru Baraza lako tumefanya kazi kubwa sana yakisheria ambayo tulipaswa kuifanya leo, Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu naomba kutoa ahadi kwako kwamba tutahakikisha maagizo na maeelekezo yote yaliyotolewa kuanzia kamati ya Fedha na Mkaguzi wa Serikali pamoja na Viongozi tutayasimamia kikamilifu ili kuhakikisha Halmashauri yetu inapunguza hoja. Pia nichukue furusa hii kipekee kumshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupendezwa kuniamini kuendelea kubaki katika Halmashauri hii, Hii inatokana  na ushirikiano mkubwa wa Madawani katika kufanya kazi “Alisema Johnson

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude, Amesema kuwa ataendelea kutoa Ushirikiano mkubwa kwa Baraza la Madiwani katika usimamizi wa ukusanyaji wa Mapato ili kuhakikisha Halmashauri kuwa na Hati safi kila Mwaka wa Fedha.

Aidha Mkuu wa Mkoa Ameitaka Halmashuri kubuni zaidi vyanzo vya Mapato amabavyo vitaifanya Halmashuri kuwa na Mapato Makubwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA AJIRA

    September 11, 2023
  • MWENGE WA UHURU UMERIDHISHWA NA MIRADI KISHAPU.

    July 27, 2023
  • SHUGHULI ZA UZALISHAJI KATIKA MGODI WA MWADUI ZA ZINDULIWA

    July 17, 2023
  • WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO ATEMBELEA MGODI WA ALMASI MWADUI

    June 30, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa