• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

RC MNDEME AMEAGIZA UJENZI WA BWAWA JIPYA LA MGODI WA ALMASI MWADUI LIJENGWE KWA KIWANGO BORA

Posted on: May 2nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, amefanya ziara katika Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu, na kuagiza ujenzi wa bwawa jipya ambalo linajengwa kwenye Mgodi huo, lijengwe kwa kiwango cha juu ili kusijetokea tena ajali ya kupasuka na kuleta madhara kwa wananchi.

Novemba 7 mwaka jana (2022) bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui la kuhifadhi maji tope, lilipasuka kingo zake na kisha tope kuvamia makazi ya watu na kuleta madhara ya kupoteza mali zao, mashamba, nyumba kufunikwa, visima vya maji, lakini hakikutokea kifo hata kimoja.

Mdeme akizungumza katika ziara hiyo leo Mei 2,2023 amesema ametembelea Mgodi huo, ili kuona namna shughuli za uzalishaji madini hua zinafanyika,pamoja na kuona hatua ambayo wamefikia ya ujenzi wa bwawa jipya, na ulipaji fidia kwa wananchi.

"Katika ujenzi wa bwawa jipya ambalo mnaendelea kulijenga hivi sasa naagiza Mamlaka zote ambazo zinahusika wakiwamo NEMC, OSHA,Bonde mhakikishe linajengwa kwa kiwango cha juu ili kusije tokea ajali nyingine," amesema Mndeme.

"Bwawa hili likianza kutumika kuwe kunafanyika ukaguzi wa mara kwa mara pamoja na marekebisho ili kuchukua tahadhari na lenyewe lisije pasuka, mjifunze kutokana na makosa," ameongeza Mndeme.

Katika hatua nyingine Mndeme amewapongeza Mgodi huo kwa kulipa fidia wananchi ambao walipata madhara dhidi ya bwawa lililopasuka pamoja na kuwapatia huduma zote, huku akiagiza kwa wale 47 ambao watawajengea nyumba wazijenge nyumba za kisasa.

Aidha, amewataka wananchi ambao wanaishi jirani na Mgodi huo kuacha mara moja tabia ya kuvamia kwa ajili ya kuiba Mchanga wa madini, bali wafuate taratibu za kuomba Lesseni za uchimbaji na siyo kuvamia eneo la mwekezaji.

Naye Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Ayoub Mwenda, amesema tangu kupasuka kwa Bwawa la Mgodi huo la kuhifadhia Maji machafu wameshalipa fidia wananchi walioathirika asilimia 96, na mwezi June watawajengea nyumba waathirika 47 na pia waliopoteza mashamba watawafidia chakula.

Amesema katika hatua ambayo umefikia ujenzi wa bwawa jipya la kuhifadhia maji machafu ni asilimia 46 na hadi kufikia Julai mwaka huu litakuwa limekamilika, na Mwezi Agost ndipo wataanza Rasmi shughuli za uzalishaji wa Almasi.

Meneja ulinzi katika Mgodi huo Zephania Mwashitete, amesema Mgodi umeshajipanga kuimarisha suala la ulinzi, kwa kujenga uzio, kuweka CCTV kamera pamoja na Fiber wire ili kuzuia wananchi wasivamie ndani ya Mgodi huo.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA AJIRA

    September 11, 2023
  • MWENGE WA UHURU UMERIDHISHWA NA MIRADI KISHAPU.

    July 27, 2023
  • SHUGHULI ZA UZALISHAJI KATIKA MGODI WA MWADUI ZA ZINDULIWA

    July 17, 2023
  • WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO ATEMBELEA MGODI WA ALMASI MWADUI

    June 30, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa