Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, amezindua mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria wilayani Kishapu, ambao utanufaisha vijiji viwili vya Bupigi na Butungwa na kuhudumia zaidi ya Wananchi 2000.
Mndeme amezindua mradi huo leo Aprili 27, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana Aprili 26.
Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji, amewataka wananchi kuitunza miundombinu yake ili ipate kuwahudumia kwa muda mrefu huku akiagiza Jumuiya za watumiaji maji kuhakikisha wanausimamia vizuri na kufanya matengenezo ili wananchi wasikose huduma ya maji.
Amesema Rais Samia chini ya utawala wake amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya maji na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono katika utawala, ili aendelee kuwaletea maendeleo.
"Kabla ya Muungano wananchi wananchi wengi walikuwa wakitumia maji ya kwenye mabwawa, visima na mito, lakini baada ya Muungano hadi sasa wananchi wanatumia maji safi na salama yakiwamo ya Ziwa Victoria na leo tumezindua mradi mkubwa wa maji hapa Kishapu," amesema Mndeme.
Aidha, amesema katika mradi huo wa majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria ambao ameuzindua leo katika kijiji cha Bupigi ameagiza viongozwe zaidi vituo vya kuchotea maji ili kutekekeza adhima ya Rais Samia ya kumtua ndoo kichwani mwanamke na kumpunguzia umbari mrefu wa kufuata maji.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Kishapu na Watanzania kwa ujumla, kuendelea kuuenzi Muungano kwa kudumisha Amani, upendo pamoja na mshikamano.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amesema Serikali wilayani humo wataendelea kuuenzi Muungano,huku akimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naye Meneja Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira wilayani Kishapu Mhandisi Dicksoni Kamanzima, amesema mradi huo wa Bupigi-Butungwa utanufaisha wananchi wapatao 2,000 na kuondokana na adha ya kutafuta maji umbari mrefu, huku akiahidi kutekeleza agizo la kuongeza vituo vya kuchotea maji.
Nao baadhi ya wanawake wa Bupigi wilayani Kishapu, wameipongeza Serikali chini ya Rais Samia kwa kuwatekelezea mradi huo wa majisafi na salama, ambao umewaondolea adha ya kutumia maji machafu na kutopoteza muda wa kufuata maji masafi umbali mrefu.
Aidha Mkuu wa Mkoa amemtaka Meneja Ruwasa kusambaza maji katika Vitongoji vyote vilivyopo ndani ya kijiji cha Bupigi na Butungwa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa