Na Ofisi ya Habari, Kishapu
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.
Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.
Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa